Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto walipokuwa katika mkutano wa kisiasa uwanja wa Serani, Mombasa. Katika mkutano huo walimpokea rasmi aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha Wiper chake Kalonzo Musyoka, Bw Hassan Omar, katima chama cha Jubilee.

Bw Omar, ambaye alikuwa seneta wa Mombasa aliwania ugavana lakini akashindwa na Hassan Joho wa chama cha ODM. Chama cha ODM na Wiper ni miongoni mwa vyama vinavyounda muungano wa upinzani wa National Super Alliance (Nasa).