Kiungo wa timu ya daraja la kwanza nchini Scotland ya Inverness, Liam Polworth ametoa kali ya mwaka baada ya kumshindilia kocha wake ngumi wakati wakiwa katika mechi. Kocha Scott Kellacher alilazimika kujilinda kwa kila namna wakati Polworth akimshambulia akiwa katika benchi. Kabla ya kumshambulia kocha wake, Polworth alifunga bao la pili na mechi iliisha wakishinda kwa mabao 3-1.

Hasira za Polworth ,22, ziliibuka baada ya kocha wake kumtoa nje na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine wakati timu yao ilipishinda dhidi ya Highlanders katika michuano ya Kombe la Irn-Bru hatua ya robo fainali.

Polworth alitoka moja kwa moja hadi katika benchi na kuanza kumlaumu kocha wake kuwa pamoja na kufunga bao, bado alimtoa nje. Kocha wake alipojaribu kumuelewesha, alianza kumshambulia kwa ngumi za kutosha hadi waliokuwa katika benchi kuingilia na kuamua ugomvi huo.