Mshambuliaji nyota wa Liverpool Mohamed Salah amefunga mabao mawili na kuiwezesha timu yake ya Misri kushinda 2-1 dhidi ya Congo na moja kwa moja kukata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwakani nchini Russia.

Ushindi wa Misri unaifanya kuwa timu kinara kundi walilo Uganda, timu anayoichezea mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.Bao la pili la Salah limepatikana katika dakika ya 90+5 na kuifanya Misri kurejea Kombe la Dunia baada ya miaka 28. Wapenda soka wa Misri hawakulala usiku kucha wamekuwa wakisherekea mitaani.

Uganda inabaki katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 8 na kufuatiwa na Ghana yenye 6 huku Congo sasa ikishika mkia ikiwa na pointi moja. Egypt (4-2-3-1): El Hadary, Fathy, Abdul Shafy, Hegazi, Rabia, Elneny, Gomaa (Trezeguet 55), Hamed, Salah, Koka (Gamal 77), Sobhi (El Mohamady 87) Unused

subs: Samir, Zakaria, Kahraba, Ashour, Morsy, Ekramy, Al Shenawy, Gaber, Gabr. Booked: Salah Goals: Salah 63, 90+5 Congo (4-2-3-1): Mouko, Badila, Etou, Itoua, Mayembo, N’Dinga, Oniangue, Bahamboula (Ndockyt 84), Bifouma, Saint-Louis (Gandze 90+2), Delarge (Moutou 71).

Unused subs: Kifoueti, Kibamba, Bissiki, Dore, Illoy-Ayyet, Pambou, Avounou, Mafoumbi, Baudry. Bookings: Badila, Etou Referee: B. Gassama