Image result for mkuchika georgeMteule katika wizara ya utumishi, George Mkuchika akiongea kwa mara ya kwanza baada ya uteuzi, amesema yeye ndie anahusika na watumishi wote wa serikali katika nchi hii pia kuzuia na kupambana na rushwa pamoja na maadili kwa viongozi wa umma.
 
Amesema katika kipindi chake cha uwaziri, anawapa ujumbe watumishi wa umma kuwa, wananchi wanapofata huduma maofisini, wawakute watumishi wakiwa ofisini na kuwaonya watumishi wanaofika kusaini maofisini na kutoka kwa kisingizio cha kunywa chai.
 
Amesisitiza atalala nao mbele watumishi wote ambao hawashindi maofisini kwao ili kila mtumishi wa umma alipwe mshahara kulingana na kufanya kazi muda wote, amedai watumishi wengi wanalipwa mshahara kamili kwa kufanya kazi nusu au robo.
 
 
Kuhusu kupandishwa madaraja, amesema yatazingatiwa hasa kulingana na uwezo wa kifedha wa serikali kwani kumpandisha mtu maana yake fedha zinahitajika, pia amesema ataongea na waziri wa elimu, somo la Rushwa lianze kufundishwa kuanzia chekechea kwani watu wengi wanaotoa Rushwa ni kwa sababu ya kutokujua kwamba huduma wanazopata ni haki yao na hawapaswi kutoa Rushwa.