Dar es Salaam. Mkali wa bongo fleva Diamond Platnumz ameendelea kupeleka mbali muziki wake kwa kufanya kolabo za kimataifa.
Safari hii Diamond ameonekana kuvuka mipaka akitarajia kuachia ngoma mpya aliyoshirikiama na rapa wa Marekani Rick Ross.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Meneja wa Diamond, Babu Tale ameweka video inayomuonyesha msanii huyo akiwa na Rick Ross wakirekodi video.
Tale aliandika, “Kuthubutu ni sehemu ya kufanya,dhamira yetu ni kuupeleka muziki wa bongo fleva mbele, kikubwa dua zenu.”
Video hiyo inaonekana kutengenezwa Miami, Marekani.
Siku chache zilizopita nyota huyo alipata tuzo ya mwanamuziki bora wa Afrika Mashariki zilizotolewa na Afrimma.

Chanzo;Mwananchi