Katika dirisha lililopita la usajili kati ya usajili ambao uligonga vichwa vya habari ilikuwa ni wa Phellipe Coutinho, Coutinho alikuwa akihitajika Barcelona na inafahamika kwamba walijitahidi sana kumpata wakashindwa.

Kulikuwa na taarifa nyingi lakini kubwa ni kwamba Liverpool hawakutaka kumuona Coutinho akaondoka na inadaiwa walikuwa wakipandisha ada yake kila siku hadi ikafikia £200m.
Habari za Coutinho zimeibuka upya na sasa taarifa kutoka Hispania zinasema kwamba mchezaji huyo ataitumikia Liverpool kwa nusu msimu na itakapofika mwezi January atajiunga na klabu ya Barcelona.

Habari ya Coutinho leo ndio imechukua nafasi katika vyombo vya habari nchini Hispania na inadaiwa kwamba tayari kiungo huyo ana makubaliano na Liverpool na wamekubali kumuachia mwezi January.

Countinho inafahamika wazi kwamba anapenda kwenda kujiunga na Barcelona na tayari alishaomba kuhamia klabu hiyo lakini baada ya Liverpool kumbania kiungo huyo alikosa raha na kupata msongo wa mawazo uliomuweka nje ya uwanja.

Hii inaweza kuwa wiki mbaya kwa Liverpool kwani habari ya Coutinho imekuja wiki ambayo Sadio Mane ameumia huku wakikabiliwa na mchezo mgumu katika ligi ya Epl dhidi ya Manchester United.