Andre Silva alifunga moja kati ya mabao mawili wakati Ureno wakiipiga Switzland bao 2 na hii inamfanya mshambuliaji huyu kuhusika katika mabao 10 kwenye michezo 10 ya timu ya taifa ya Ureno.

Na ushindi wao wa leo ni mafanikio mengine kwao na kwa mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo kwani Wareno wanakuwa wamekata rasmi tiketi ya kushiriki kombe la dunia,Hii ni mara ya 9 mfululizo kwa Ureno kushiriki kombe la dunia huku safari hii wakiwa wamefunga jumla ya mabao 32 na wakiwa na clean sheets katika michezo 7.Timu ya taifa ya Ufaransa nayo imewapiga Belarus bao 2 kwa 1 na kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia huku wakiweka rekodi ya kutopteza mchezo hata mmoja katika uwanja wao wa nyumbani wakati wa mechi za kufudhu.Kule Ubelgiji nako watoto wawili kutoka familia moja ya mzee Hazard walishirikiana kuendeleza utemi wa Ubelgji, huyu ni Eden Hazard alyefunga mara mbili huku Thorgan akifunga moja na Lukaku akimalizia la nne dhidi ya Cyprus.
Kwa ushindi huu wa mabao manne huku magoli mawili kutoka kwa Eden Hazard yanmfanya hadi sasa kuhusika katika mabao 9 ya Ubelgiji katika michezo 10 akigunga manne na kuassist 5.
Michezo mingine ya Group H timu ya taifa ya Ugiriki ilishinda mabao 3 kwa 0 dhidi ya Gibrtar huku mabao ya Ugiriki yakiwekwa kimiani na K Mitroglou (2) na Torosidis.Timu ya taifa ya Uholanzi imekwama kufuzu kwa michuano ijayo ya kombe la dunia licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Sweden lakini haikutosha kuwapeleka kombe la dunia.