Kushoto Waziri wa Mifupo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiongea na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo hawapo katika picha, katika Ofisi a Dar es Salaam mara baada ya kuripoti, katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Abdalah Ulega kulia ni Dkt. Yohana Budeba katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uvuvi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiweka sahini katika kitabu cha wageni cha Wizara hiyo mara maaba ya kuripoti.
Kushoto Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara Mpya ya Mifugo na Uvuvi upande wa mifugo Dkt. Maria Mashingo kulia, wakati wa mazungumzo mafupi mara baada ya kuripoti katika Wizara hiyo.
Katika picha sehemu ya baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakifurahia jambo mara baada ya kuwapokea Mawaziri waliopewa dhamana ya wizara hiyo mpya, hawapo katika picha.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega Akimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo Mpya Mhe. Luhaga Joelson Mpina hayupo katika picha mara baada ya Mawaziri hao kuripoti katika Wizara hiyo katika Ofisi za Dar es Salaam.