Mkuu wa Mkoa Wa mjini Magharibi Zanzibar Ayoub Mohamed Mahmoud amezungumza na waandishi wa habari kutoka Dar es Salaam ambapo amezungumzia mambo yatakayofanyika siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere na kilele cha Mwenge.

Amesema wamepokea kwa mikono miwili na kwa furaha jambo hilo kwani ni mara ya kwanza kufanyika visiwani Zanzibar na kuna mambo mauhimu yatafanyika siku hiyo.

Aidha amesema Mgeni rasmi katika sherehe hizo atakua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ambapo pia atashiriki Misa ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa.

“Tutafaya misa ya kumbukumbu ya kwenye Kanisa la Roman Catholic Shangani lilipo Kisiwani hapa Zanzibar na baada ya hapo Rais Magufuli atatembelea maonesho yaliondaliwa” amesema

Hata hivyo kasema baada ya shuguli hizo jioni kutakua na burudani itakayo ongozwa na msanii Daimond na wengine ambapo amesema pia swala la ulinzi limeimarishwa.