Tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli watu wengi wamekuwa wakihoji ni nani hasa anayenufaika na huu utawala..
Malalamiko mengi yamekuwa yakitolewa na watetea mafisadi wa ufipa kwamba zama za Rais Magufuli kila mtu anaisoma namba wala hamna mwenye nafuu.

Lakini uchunguzi niliofanya umenipa majibu tofauti kabisa.
Watu wafuatao wanakula mema ya Rais Magufuli kwa sana tu na hawataki kabisa atoke madarakani.

1. Wamachinga
Kabla ya Rais Magufuli kuwa machinga ilikuwa ni balaa tupu ,kila siku walichezea vipigo na kuchukuliwa bidhaa na mgambo.
Leo ndani ya utawala wa Rais Magufuli wamachinga wanafanya biashara ndani ya jiji bila shida yoyote.
Kwa nini wasimpende Magufuli?

2. Wakulima
Chini ya utawala wa Rais Magufuli kodi zote za ajabu ajabu zimefutwa hivyo kuongeza tija kwa wakulima.
Mazao ya chai ,korosho, Pamba, mpunga, tumbaku yalikuwa na kodi zaidi ya kumi!!!
Sasa kwa nini wasimpende Rais Magufuli??

3. Wafugaji
Kabla ya Rais Magufuli kuwa mfugaji ilikuwa adhabu tosha.
Ukipeleka kuuza Ng’ombe mnadani unakutana na kodi ya kwato na pembe!!

Chini ya Magufuli hizo kodi zote zimefutwa. Sasa wafugaji wanafanya biashara zao kwa raha na kujiongezea kipato.

Pia watu wa vijijini walikuwa wananyanyaswa sana wakienda kwenye huduma za serikali ,lakini sasa hivi wanaheshimika na kuhudumiwa vizuri.

Sasa hutaki wampende Magufuli ili wakupende wewe mtetea mafisadi?

Watetea mafisadi wote wajue kupambana na mtu ambaye siyo Mnafiki inahitaji timing na akili nyingi .

Magufuli siyo mnafiki ,nyeupe anasema nyeupe na nyeusi anasema nyeusi.

Wanasiasa wengi wamezoea kusema nyeusi ni nyeupe na nyeupe ni nyeusi.
Nawambieni watapata shida enzi ya Magufuli.

Asante Jakaya Kikwete kwa kutuachia Rais Magufuli mafisadi wanafungasha virago wenyewe na kuiacha Tanzania yetu.