Ndege zisizo na rubani (Drones) ni moja ya Teknolojia ambayo inatajwa kukua kwa kasi kutokana na mahitaji yake kuwa makubwa na kumekuwa na matoleo tofauti tofauti ambayo yametoka yanayoweza kutumika katika sehemu tofauti, Tumeshudia Drones zikitumika kushoot Video, kusambaza bidhaa, kutoa huduma ya kwanza na hizi mpya ambazo zenye uwezo wa kubeba mtu kama abiria,

 

      Sasa Bad Newz ni kwamba, Tafiti zinaonyesha kuwa Drone zinaaweza kudukuliwa kirahisi. Drone ni ndege ambazo zimetengenezwa kwa Plogramu ambazo hutumia Comand katika kuzitumia, Tafiti zinaonyesha kwamba kuna kirusi ambacho kinaitwa MALDRONE, chenye uwezo wa kubadilisha komand zilizopo kwenye Drone yako pamoja na simu/ kifaa chako unachotumia kuendesha Drone hiyo.

 

             Moja ya njia ambazo zinapelekea kirusi hicho kudukua Drone yako, hutumia Command za uongo ambazo zinauwezo wa kuingiliana na Drone yako na kuweza kusababisha uharibifu kwa kuidondosha hiyo Drone au kuipoteza muelekeo.