Rais John Magufuli na kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani, Mtukufu Aga khan wamezungumza mambo makubwa matatu yatakayo saidia maendeleo ya Tanzania.

ELIMU kuhusu elimu Rais Magufuli amesema Mtukufu Aga Khan na taasisi yake wataanzisha ujenzi wa chuo cha kikuu kikubwa huko Arusha na tayari wamesha pata eneo na ujenzi huo utaanza ndani ya miezi sita.

VYOMBO VYA HABARI baada ya mazungumzo na Rais Magufuli mtukufu Aga Khan amesema haamini kama vyombo vya habari ni kujikita kwenye habari za kisiasa pekee lakini wana wajibu mpana wa kujikita kwenye maswala ya maendeleo hivyo hivyo watajikita katika kuandaa waandishi.

AKDN Mtukufu Aga Khan pia ni kiongozi wa mtandao wa maendeleo ambao unatoa huduma mbalimbali duniani ambapo kwa hapa nchini mtandao huo unataoa huduma za kiafya, bima ,elimu na mikopo kwa wajasiriamali na kusaidia kilimo haswa kwa wakulima vijijini.

Ziara ya Mtukufu Aga khan inalenga kuimarisha biashara baina ya serikali na taasisi yake ambayto ina uwekezaji mkubwa hapa nchini.