Mkuu wa wilaya ya Chunya, Bi. Rehema Madusa ameingoza Kamati ya Ulinzi na Usalama kuteketeza nyumba zaidi ya 900 za wananchi ambao wamevunja sheria kwa kuvamia na kuishi ndani ya hifadhi ya misitu ya asili iliyopo tarafa Kipembawe Chunya.

Kufuatia zoezi hilo la kuwaondoka watu hao waliovamia hifadhi hizo lililofanywa na Kamati ya Ulinzi kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu nchini, TFS, zaidi ya kaya 1000 zimekosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuchomwa moto.

Meneja wa wakala wa huduma za misitu (TFS) Grace Wille, wilaya ya Chunya amesema kuwa katika tarafa ya Kipembawe kuna misitu zaidi ya saba inayohifadhiwa, lakini misitu hiyo imevamiwa na makundi ya watu ambao wanaendesha shughuli za kiuchumi.

Amesema kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kwamba zoezi hilo la kuwaondoa ambalo limeanza leo litakuwa ni endelevu.