Rais wa nchi ya Panama, Juan Carlos Varela ametangaza siku ya Jumatano kuwa siku kuu baada ya nchi hiyo kufuzu kushiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanaza kuanzishwa kwake mwaka 1978.

Kupitia mtandao wakijamii wa Twitter,Carlos Varela‏ ameandika, “Sauti za watu zimesikika…Kesho ni sikukuu ya kitaifa.”
Timu hiyo ya taifa ya Panama iliifunga Costa Rica jumla ya mabao 2-1 mjini Panama City hapo jana siku ya Jumanne na hivyo kufuzu michuano hiyo ambayo wananchi wan chi hiyo walikesha usiku kucha wakisherehekea.


Rais amesema wafanyakazi wa umma na wale wa makampuni ya watu binafsi na wanafunzi wote watapumzika kwa siku moja na hivyo shule hazitafunguliwa ikiwa ni ishara ya furaha yao.

Panama inaungana na Mexico, Costa Rica kushiriki kombe la dunia mwakani huku Marekani ikishindwa kufuzu katika kundi hilo la Amerika ya Kaskazini na Kati.