Mkuu wa Mkoa Wa mjini Magharibi Zanzibar, Ayoub Mohamed Mahmoud, amempokea Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ikiwa wamewasili Kisiwani Zanzibar leo.

 

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika Uwanja wa ndege wa Zanzibar akiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema anayo furaha kumkaribisha pamoja na wageni wengine wote waliofika kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Julius Nyerere namaadhimisho ya kilele cha mwenge.

” Ndugu Mkuu wa Mkoa karibu sana Zanzibar hapa ni salama jisikie uko huru, nimefurahi ujio wako katika shughuli zitakazo fanyika kesho na tutakua pamoja hata katika tukio la usiku la burudani ambapo Msanii Diamond atatumbuiza” amesema.

Aidha wageni waliombatana na Makamu wa Rais na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge ajira na Walemavu Jenesta Muhagama pamoja na naibu wake Anthony Mavunde.

Makonda amesema baada ya shuguli hizo za kesho kumalizika atakuwepo kwenye burudani ya usiku itakayotolewa ikiongozwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz.