Ryan Giggs ndio mchezaji ambaye anaongoza kucheza katika mtanange wa North-West Derby. Amecheza jumla ya mechi 48 tangu alipoanza kuitumikia United mwaka 1990 mpaka 2014 alipostaafu.
Nahodha mstaafu wa Liverpool, Steven Gerrard pamoja na wakongwe wawili wa United, George Wall na Sandy Turnbull ndio wafungaji bora wa muda wote wa North-West Derby.
Wote wamefunga magoli 9 kila mmoja.
Mchezo huu utakuwa wa pili katika dimba la Anfield unaowakutanisha Jurgen Klopp na Jose Mourinho.
Makocha hawa wawili wameshakutana mara 7, Mourinho ameshinda mara 1 tu, Klopp ameshinda 3 na sare 3.
Kocha wa zamani wa Liverpool Graume Souness alishauriwa kumnunua mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Eric Cantona pamoja na kipa wa zamani wa Manchester United Peter Schmeichel lakini akawatosa.