MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Barcelona, Oscar Grau ametoa kauli ambayo inaweza kuwatikisa Wanaliverpool baada ya kusema kuwa wanajipanga kurejesha mchakato wa kumwania kiungo wa timu hiyo, Philippe Coutinho katika usajili wa Januari. Barcelona ilishindwa kumsajili mchezaji huyo katika dirisha la usajili mkubwa lililopita baada ya kumpoteza Neymar aliyetimkia Paris Saint-Germain.

 

Coutinho amekuwa akiendelea kuhusishwa kuwaniwa na vigogo hao wa Hispania kwa dau la pauni milioni 118. Kigogo huyo amesisitiza kuwa hawajakata tamaa ya kumwania mchezaji huyo licha ya kuwa Liverpool imekuwa ikionyesha haina nia ya kumruhusu kuondoka. “Tutakuwa tayari kumsajili Coutinho wakati wa majira ya mvua, au mchezaji mwingine yeyote ambaye tutakuwa tunamhitaji,” alisisitiza kigogo huyo na kuendelea: “Tunatakiwa kusahau habari za ada ya uhamisho wa Neymar, hayo ni mambo ya msimu uliopita.” BARCELONA, Hispania