Ndege ya mizigo imeanguka katika bahari ya taifa la Ivory Coast , muda mfupi baada ya kuondoka mji mkuu wa Abidjan huku watu watatu wakidaiwa kufariki na wengine wakijeruhiwa.

Mabaki ya ndege hiyo aina ya Turboprop yalisombwa hadi katika ufukwe ambapo waokoaji walionekana wakiwatibu watu walionusurika katika ajali hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa ikibeba mizigo ya jeshi la Ufaransa, kulingana na habari za mtandao wa Koaci.
Inasemekana kuanguka wakati wa mvua kubwa karibu na bandari ya Bouet.