Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amewataka vijana kuacha ngono zembe badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya nchi.

Amezungumza hayo leo hapa Visiwani Zanzibar alipokuwa kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na kilele cha Mwenge ambapo ameeleza vitu vingi ikiwemo mambo ya Viwanda.

Hata hivyo amesema kuna baadhi ya watu wanataka maadhimisho ya Mwenge yafutwe jambo hilo haloiwezi kukubarika na wanaosema hivyo wasahau jambo hilo.

“Nataka watanzania watambue umuhimu wa Mwenge kwa sababu Mwalimu Nyerere aliapata shida hadi kupatikana kwa mwenge wa uhuru hao wanaosema tuwazomee tuwapuuzie na hatuwezi kuufuta”amesema.

Aidha Rais amewataka Viongozi wafuate nyayo za Mmwalimu kwani viongozi wa saivi wengi wamejaa na tamaa migogoro na kutumia fedha vibaya ambapo wanasahau kuna watanzania wanahitaji huduma za kijamii.

“Sijui sisi watanzania nani katuroga viongozi wa saivi hakuna anayeweza kuwa na tabia kama za mwalimu kipindi hicho angetaka hata kumiliki Bahari ya Msasani angeweza ila alikuwa na roho nzuri ila viongozi wa saivi wengi sana wanamiliki tena vitu hivyo inasikitisha sana”

Amesema wataendelea na maadhimisho hayo kila mwaka itakapofika tarehe kama ya leo na atakaye sema maadhimisho yafutwe basi atashughuliki bila shaka.