Baada ya wiki kadhaa Zari na mpenzi wake Diamond Platnumz kudaiwa kutokuwa katika maelewano mazuri, leo October 13 amewasili jijini Dar es salaam akitokea Afrika Kusini na kupokelewa na mlinzi wa Diamond, Zari amekuja Tanzania kwa ajili ya uzinduzi wa Danube ya Mlimani City.

 

Wakati bado haijafahamika kama ni kweli Zari ameachana na Diamond, leo hii mrembo huyo ametua nchini ikiwa ni mara ya kwanza tangu sakati lake na mzazi mwenzake Diamond litokee amekua Afrika kusini. Aidha kumekuwa na maneno yanaandikwa na kujidili juu ya wapenzi hawa kwenye mitandao ya kijamii kwa kipindi chote.