MTU mmoja nayetuhumiwa kwa mauaji ya wanafunzi watano na mlinzi mmoja katika shule ya Sekondari ya Lokichogio huko Turkana nchini Kenya ameuawa na wakazi wa kambi ya wakimbizi ya Kakuma.

Mtuhumiwa huyo alikuwa amekamatwa na polisi kabla ya wakazi hao kuvamia Kituo cha Polisi cha Kakuma na kumchoma moto.

Kamanda wa Polisi wa Turkana Ronad Opili amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtu huyo alikamatwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma alipokuwa akijaribu kukimbilia Sudan Kusini.

“Wanafunzi kadhaa wamejeruhiwa. Hatuwezi kuthibitisha idadi yao hadi tupate taarifa za hospitali,” amesema Kamanda Opili akizungumza na waandishi wa habari.