Watanzania tunapenda kulalamika kila kitu… vitu vingine vidogo tunavikuzaa na kuvifanya vikubwa saa nyingine kuharibu kabisa.. . . Mwacheni Zari apige kazi… Kwani Leo ndo mmemuona? Amekuwa balozi wa Danube zaidi ya miaka miwili hamjasema Leo ghafla ooh Danube mnapendelea.. Mara ooh Uganda athaminiki kama Tanzania… Sasa hiyo thamani si ni sisi watanzania tumempa? Tumemkaribisha, tukampa huo umaarufu yeye kautumia kujiingizia kipato.. Kwani kosa lake nini hapo? Makampuni yameheshimu maoni yetu… Yakaona kumbe Zari anafaa kwa kazi zao!! . .

 

             Mnadhani akili zake ziko kama za wengine? Zari anamaanisha biashara..Maisha yake, watoto wake, Account yake ya IG mtu unatamani kufanya nae biashara.. Hata kama yuko fake, but kajitengenezea mazingira ya kupokea mikataba/biashara! Huo ndo ukweli wenyewe..Haya nyie original kipi mnafanya kwa watanzania..? Account haijulikani wewe hasa ni nani, full kachumbari, drama za kijinga nani akupe deals? . . Hatupendani, kutwa majungu, kupigana vikumbo hata hizo nafasi ukisikia fulani kapewa utamfanyia fitna mpaka akose…hatupendi kuona mwenzetu anainuka!! Mabwana tunachukuliana hovyo sembuse hizo fursa za kazi? . Mfanyabiashara anachagua afanye kazi na nani ambaye atamwingizia faida…

Awe mtanzania au nchi nyingine…akina Flaviana Matata wanafanya kazi US na wengine kibao wana mikataba nje ya nchi.. Kwavile siyo wa nchi husika hawafai kufanya kazi nchi hizo mpaka wazawa? . . Tuacheni teams na chuki zisizokuwa na maendeleo… GSM wanafanya kazi na watanzania akina Ommy Dimpoz ni wa Congo??? Joti je?? Wema alishawahi kufanya kazi nao pia nk. Kwa vile ni Zari??.. Na hizo campaign ghafla ndo mmeamka Leo??

 

Zari anajua kujipanga, Ana team inayompa support pamoja na sisi watanzania tuliomfikisha hapo, Either unampenda au unamchukia ndo mafanikio yake unayoyaona Leo, kageuza imekua fursa… . Na kawanyorosha anajua ku grab opportunities… Na iwe fundisho kwa wengine tengeneza mazingira yako na unapopata deals usipige kelele…sign contract kwanza ndo uongee… Kuna wengine wajanja wanajua kuona fursa kwa jicho la tofauti na mazoea…anakuwahi unabaki Ooh sijui naonewa hapana. Ni kazi… Kila mtu ana upeo wake aipateje kaz