MSANII na mwanamitindo Hamisa Mobeto amefunguka kuhusu uhusiano wake na Zari kuwa ana tatizo na mke mwenzake huyo kuwa hamchukii kwa sababu watoto wao ni ndugu. Alisema mwanzo hakuwa anamkubali. Alipoulizwa uhusiano wake na mke mwenza huyo alifunguka na kusema:

 

          Mimi sina tatizo naye kwa sababu watoto wake ni watoto wangu kwa hiyo mimi sina tatizo ipo siku watoto ( wa Zari) watataka kuja kumuona ndugu yao au huyu wangu atataka kuwaona ndugu zake, tuwaruhusu tu, kwa sababu sisi wote ni wake wa mtu mmoja, kwa hiyo hatupaswi kuwa na matatizo, ila kwa mimi sina tatizo naye,” alisema Hamisa Mobeto