MWANAMITINDO Hamisa Mobeto amefunguka kuhusu uhusiano wake na mjasiriamali Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuwa hana tatizo na ‘mke mwenzake’ huyo na hamchukii kwa sababu watoto wao ni ndugu na yupo tayari kuwa nyumba ndogo. Alisema awali hakuwa anamkubali mke mwenziye huyo lakini kwa sasa hana budi kumkubali.

Mimi sina tatizo naye kwa sababu watoto wake ni watoto wangu kwa hiyo mimi sina tatizo ipo siku watoto wale (wa Zari) watataka kuja kumuona ndugu yao au huyu wangu atataka kuwaona ndugu zake, tutawaruhusu tu kwa sababu sisi wote ni wake wa mtu mmoja, kwa hiyo hatupaswi kuwa na matatizo, mimi sina tatizo naye,” alisema Hamisa Mobeto.

Kuhusu madai ya kupewa shilingi 70,000 kila siku yaliyosemwa na mzazi mwenzake hivi karibuni, Mobeto alifafanua: “Kama mtu mzima lazima ujue kuwa mwanamke mwenye mtoto anahitaji nini na nini, unapokuwa na mpenzi wako au mke wako huwezi kushindwa kumpa hiyo elfu sabini au laki moja, kwanza mimi na yeye tulikubaliana kuzaa siyo kama mimi nilimlazimisha hapana, halafu mpaka mimi nakwenda mahakamani ni kwa sababu nyuma yangu kulikuwa na watu wananisimamia ndiyo maana nikapeleka hili suala mahakamani ili malezi ya mtoto yaje, basi. Yeye alimleta mwanasheria wake wakakutana na mwanasheria wangu kwa hiyo haya mambo tuyaache kwanza,” alisema Hamisa.