Baba wa msanii aliyezaa na Hamisa Mobeto, Abdul Juma. BAADA ya hivi karibuni mwanamitindo Hamisa Mobeto kumpeleka mahakamani msanii wa Bongo Fleva kwa madai ya malezi ya mtoto aliyezaa naye, baba wa msanii huyo, Abdul Juma ameibuka na kusema hata iweje, yeye atakufa na mkwewe huyo kwani hayo mengine ni ya kwao, hayamhusu.

Mwanamitindo Hamisa Mobeto. Akipiga stori na Risasi Jumamosi, mzee Abdul alisema anachojua yeye, Hamisa ni mkwe wake aliyempa heshima na kumtambua kama baba mkwe wake hivyo hata mwaliko aliompa wa kwenda kwenye sherehe ya mwanaye huyo aliyepewa jina lake la Abdul atakwenda kama kawaida kama atakuwepo, hajali kama wamepelekana mahakamani wala nini.

Hayo mambo ya migogoro yao hayanihusu kwa kweli na hayawezi kunifanya nikamchukia Hamisa kwa kuwa ni ya kwao, nikiwepo Dar lazima niende kwenye sherehe ya mjukuu wangu Abdul wala sijali chochote,” alisema mzee Abdul