Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahamoud amewashukuru wananchi  kwa ushirikiano walimuonesha katika kipindi chote cha  kuanzia maandalizi hadi siku yenyewe ya tukio la kumbukumbu ya Baba wa Taifa na kilele  cha mwenge.

Akizungumza leo na vyombo vya habari hapa Kisiwani Zanzibar amesema kwa wale ambao aliwakwaza anaomba radhi lakini anashukuru shughuli ilienda vizuri na watu kuonesha uungwana.

“nawashukuru viongozi wenzangu wote wa bara na wa huku Zanzibar kwani tumeweza kufanikisha jambo hili kwa uzuri katika maadhamisho ya kilele cha mwenge wa uhuru pamoja kuadhimisha kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere” amesema.

Hata hivyo ameshukuru sana vyombovya habari vyote kutoka bara na huku visiwani kwani wameweza kufanikisha kufikisha habari ya shughuli hiyo na vyombo vyote vilivyokuwa vinarusha live kutoka kwenye tukio.