Wananchi wa Visiwani Zanzibar wakuwa wakitoka kwa furaha kubwa wanapotoka ndani ya  Meli  ya Kifahari ya Mfalme Qaboos wa Oman FULK AL SALAMAH iliyopo katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Oman.

 

 

 

 

Lengo la  kufika kwa meli hiyo ni kuimarisha umoja Amani na Upendo,a imekuja  ikiongozwa na Waziri wa Mafuta na Gesi Dkt,Mohammed Bin Hamed Al Rumhi wa Serikali ya Oman pamoja na idadi kubwa ya mabaharia na wanajeshi.

Wananchi hao wengi wao wakiwa warabu wamekua wakifurahia zawadi walizokuwa wapatiwa kwani zilikuwa tofauti tofauti ikiwemo Kanzu, tshet, kofia na skafu pamoja na mifuko ya pipi.

Aidha meli hiyo inatarajia kutia nanga jiini Dar es Salaam na baadae kuingia Mombasa, ukubwa wa meli hiyo umeweza kuwavutia wengi kwa nje na ndani ambapo ndani baadhi ya vitu vyao ikiwemo birika za kahawa ni dhahabu.