NILIWAHI KUSEMA MANENO HAYA KUWA MABINTI WANATAKIWA KUJIFUNZA KUTOKA KWA @zarithebosslady.
1) kuwa na mahusiano kwa malengo
2) kuzaa kwa malengo
3) kujua kutumia fursa ya mwanaume uliye naye.

TATIZO TUKIANDIKA MAMBO HAYA TUNAKULA MATUSI WAKATI LENGO NI KUWAAMSHA TU KUJIFUNZA.

Leo mtu anatoka anandika na kulalamika kuwa @zarithebosslady anapiga deals kubwa mbele ya wasichana warembo wa Tanzania akasahau uzuri bila akili ni kazi bure.

Hivi nimekaa nikajiuliza @diamondplatnumz ashawahi kuwa na mahusiano na mabinti wa ngapi mbona hakuna aliyewahi kupiga deals kama hizi nikagundua hawakuwa na akili za kutumia fursa kama @zarithebosslady.
Nikajiuliza ina mana wapenzi wa diamond hawakuona fursa ya kuzaa na jamaa nikagundua waliendekeza sana ujana wakahofia kuharibu usichana wao ila @zarithebosslady aliona kabisa akizaa na @diamondplatnumz hazai watoto bali anazaa asset.

Naomba niwatoea hawa @jokatemwegelo @flavianamatata @millenmagese mana hawa wanajitambua na wanapiga deals zao vizuri tena wengine mpaka nje ya nchi na tusiwatumie kama vigezo kabisa mana wao wana mambo yao ya msingi.

@zarithebosslady amefanya kitu kidogo tu ameunganisha nguvu ya mahusiano yao ndio hapo anatembea na chaki na mabinti zetu wasisahau huu ubalozi ni baina ya wapenzi @zarithebosslady na @diamond.
Watu mmekaa na @diamondplatnumz miaka 9 mmeshindwa kumtumia vizuri katoka mtu nje ya nchi kamtumia mnalalamikaje wakati miaka yote mlikuwa naye.

BEAUTY WITH BRAIN ndio wanachokosa dada zetu hawa.Wanawekeza uzuri wao katika kutafuta wanaume wanategemea nini. Mwanamke ana idadi kubwa ya wanaume aliotembea nao kuliko idadi ya kazi zake unategemea nini.

Mastaa siku hizi wa TZ wanaongoza kwa kuwa na mafekero ya kutukania watu kuliko idadi ya asset zao.

ZARI NI BRAND KUBWA:Leo jiulize msichana gani staa angeweza kujaza watu MLIMANI CITY haya makampuni yanajitambua sana

NAOMBA MWACHENI MGANDA HUYU AENDELEE KUTOA SOMO KWA DADA ZETU.

WAKATI MNANUNUA BANDO ZA KUMTUKANA YEYE ANAKATA TIKETI ZA NDEGE KWENDA KUINGIA MIKATABA MINONO YA HELA.

@zari ANAWAFUNDISHA MASTAA WETU MAANA YA NENO SHOWBIZ LESS DRAMA MORE MONEY.

ENDELEENI KUMUITA MZEE KAMA NYIE UMRI WENU UNARUDI NYUMA.
By @abby1_thebest