Mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ambaye pia ni mzazi mwenza wa Mbongo Fleva, ambao hivi karibuni ilisemekana wamemwagana kutokana na mgogoro mzito uliosababishwa na Mbongo Fleva huyo kuchepuka na kuzaa na mwanamitindo maarufu Bongo,

 

Hamisa Mobeto, hatimaye leo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wamewaziba watu midomo, baada ya kutupia video wakiwa pamoja kisiwani Zanzibar. Video hiyo iliwapa joto mashabiki na wakajikuta wamepigwa na butwaa, kwani stori zilishaenea kuwa wawili hao wameshapigana kibuti na imebaki stori, lakini baada ya wawili hao kutupia video hiyo ikajibu maswali yote kuwa wapo pamoja tena kwenye dimbwi zito la mahaba. N