Watu 7 wamefariki papo hapo na wengine 14 kujeruhiwa, baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah kugongwa na lori la mizigo wakitoka kwenye sherehe ya harusi wilayani Hanang mkoani Manyara.
Ajali hiyo ambayo imetokea usiku wa Oktoba 14, 2017 imehusisha Noah yenye namba za usajili T 744 DJQ, likiwa limebeba watu wa familia moja, kugongwa na lori aina ya semiteller lenye namba za usajili T449 CDR mali ya kampuni ya Lake Hill Paradise ya Singida, na kuleta majonzi na simanzi kwa ndugu wa marehemu