Mauro Icardi mchezaji wa kwanza kufunga hat trick kwenye Miran Derby tangu 2012 Diego Milito alipofanya hivyo.

Kila mpenda soka hapo jana alielekeza macho Sansiro ambapo vilabu viwili vikongwe Ac Millan na Inter Millan walikuwa wakikabiliana katika mchezo wa Millano Derby.

Wengi walitamani kuona battle kati ya mshambuliaji gumzo Italia Mauro Icardi dhidi ya beki anayetajwa kwamba ni kati ya mabeki visiki zaidi katika soka la sasa Leornado Bonucci.
Dakika 28 tu za mwanzo Icardi alionesha makucha yake baada ya kuweka kambani bao la kwanza lililodumu hadi mapumziko, lakini Ac Millan walirudi kipindi cha pili na kusawazisha kupitia Susso.
Mauro Icardi tena dakika ya 68 aliongeza la pili kabla ya Millan kuchomoa dakika ya 81 kupitia kwa Giacomo Bonaventura na wakaamini mpira unaweza isha kwa suluhu lakini Icardi tena dakika ya 90 akafunga kwa mkwaju wa penati.Kwa matokeo hayo sasa Ac Millan wanashika nafasi ya 10 na alama zao 12 huku Intet Millan wakibaki katika nafasi yao ya pili wakiwa wamejikusanyia alama 22 msimu huu.

 
D