Mmiliki na Mchapishaji wa jarida la picha chafu za utupu la Hustler, Larry Flynt, amekuja na mpango wa kumng’oa madarakani Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kutangaza dau nono la mamilioni.

Rais Donald Trump na Larry Flynt

Bwana Flynt kupitia tangazo lake alilotoa kwenye gazeti la Washington Post  amesema atatoa kiasi cha dola milioni $10 sawa na Tsh bilioni 22 kama zawadi kwa mtu yeyote atakayetoa  taarifa chafu kumuhusu Rais Trump ambazo zitamfanya ang’atuke madarakani.

Tangazo la Larry Flynt

Flynt, amesema kila Mmarekani anawajibu wa kumuondoa madarakani Rais Trump kwani wakichelewa basi taifa hilo litakuwa na machafuko makubwa ya kibaguzi.

“Kumtoa Rais Trump madarakani kitakuwa ni kitendo cha kiungwana, kwani miaka mitatu iliyosalia kuishi nae ni kama safari ya jangwani, hili ni jukumu letu sote wamarekani bado hatujachelewa,“amesema Flynt kwenye Tangazo hilo.