jokatemwegeloJuzi nilialikwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali ya Kidato cha nne shule ya Sekondari Migombani iliyoko Tabata. Ingawa niliomba udhuru kutokana na kutingwa nilifanikiwa kwenda baadae sana jioni na wanafunzi wakaombwa warudi niongee nao kidogo.

Hapa nikiwa na Mwalimu Mkuu wa shule tukizungumza baada ya kupitia risala ya wanafunzi. Mmoja ya vitu waliyovitaja kama changamoto ni wanaumia njaa wakiwa shuleni. Unaweza ukashangaa inakuwa je shule iko mjini na bado watoto wanalia njaa shuleni.

 

Ila tulikubaliana kutafuta njia ya kutatua changamoto hiyo na ikawa mwanga hata kwa viongozi wa jamii ya pale wakaamka na kuhakikisha watoto wetu wanasoma katika mazingira rafiki zaidi. Kama kuna mtu ana maoni zaidi ya jinsi ya kutatua changamoto hii, karibu tubadilishane mawaz