Samson Mwigamba Ajiuzulu Uongozi ndani chama cha ACT- Wazalendo

Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa ya Chama Cha ACT Wazalendo Samson Mwigamba ameng’atuka nafasi yake hiyo katika chama hicho na kubaki mwananchama wa kawaida kwa madai ya kuwa ameona kuna mambo ndani ya chama hicho hayaendi sawa.

Mwigamba amedai kuwa amejitahidi sana kuongea na viongozi wakuu wa chama hicho kuhusu mambo mbalimbali lakini ameona yamekuwa hayatendeki wala kufanyiwa kazi hivyo ameamua kufanya maamuzi hayo ili kuto pingana nao bali ameamua kubaki kama wanachama wa kawaidia ili aweze kupata nafasi ya kuhoji baadhi ya mambo ndani ya chama.