Waswahili wansema tembea ujionee mengi! Katika kijiji cha Brahmapuri kilichopo jimbo la Maharashtra nchini India chui amegeuzwa kitoweo na baba mmoja mwenye hasira kali baada ya kuua familia yake.
Chui akiwa ameuawa kwa shoti ya umeme kabla ya kufanywa kitoweo.

Chui huyo ambaye kuanzia mwezi septemba hadi Octoba mwaka huu ameua mama na watoto watatu wa familia moja, ambapo baba wa familia hiyo ameeleza kuwa alikuwa akitoka maporini na kuja kwenye kijiji hicho kwa lengo la kukamata mbuzi.

Wananchi wa kijiji hicho wamesema waliweka mitego mbalimbali ikiwemo sumu ili kumnasa chui huyo lakini walishindwa, ndipo wakachukua uamuzi wa kuweka fensi la nyaya za umeme na kumnasa chui baada ya kupigwa shoti ya umeme.

Chui huyo akiwa amefariki baada ya kupigwa shoti ya umeme.

Wananchi hao walifanikisha safari hiyo ya kumnasa chui huyo aliyefahamika kwa jina la ‘Kala’ jumamosi ya wiki iliyopita, ambapo kwa mujibu wa mtandao wa NDTv chui huyo mwezi julai alijeruhi watu wanne na kuwasababishia ulemavu wa kudumu.

Mwanaume huyo (Baba wa Familia iliyopotezwa na chui) alichukua maamuzi hayo ya kumfanya kitoweo chui huyo kwenye hitma ya mke wake aliyeuawa mwezi septemba mwaka huu ili kupoza machungu ya kupotelewa na familia yake.

“Chui huyu ameua watu wanne na kujeruhi wengine wanne hapa kijijini, awali tulitaka kumpiga risasi lakini tukaona itaweza kuleta madhara kwetu ndipo tukatumia fensi ya umeme ili kumnasa,“amesema Rajan mwanakijiji aliyeshuhudia tukio hilo.

Wananchi wa kijiji hicho walifurahishwa na tukio hilo kwani awali liliwafanya waanze kuamini imani za kishirikina.

Polisi mjini Maharashtra imethibitisha taarifa hizo kwa kusema kuwa itafanya uchunguzi wa tukio hilo kwani mpaka sasa wamefanikiwa kukamata kichwa na ngozi ya mnyama huyo.

Hata hivyo, polisi wamekiri kuwa walipokea malalamiko hayo kutoka kijijini hapo ya kuuawa na kujeruhiwa kwa watu lakini walitaka kumkamata chui huyo akiwa hai ili wamrudishe mbugani. ambapo wamesema walikuwa wanatumia mitambo ya GPS kumfuatilia.