Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu leo alikua kwenye mkoa wa Kilimanjaro kuweka baraka zake kwenye wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambapo hakuacha kuongelea ishu ya Trafiki wanavyotumia tochi zao.Mama Samia amesema “Msigeuze tochi hizi kuwa chanzo cha kuwanyanyasa Madereva na kudai rushwa, nakumbuka kuona kibonzo cha Masoud Kipanya gazetini, Trafiki kamsimamisha Dereva na kumwambia amepiga honi bila sababu za msingi kwahiyo ni kosa“
“Kipanya akaondoka na kusema….. nchi ya kuviziana, naamini kwamba hii sio taswira ambayo tunataka Wananchi wawe nayo kila wanapowaona Askari barabarani“