Majeruhi wakiokolewa.
IDADI ya watu waliouawa kwenye, mlipuko mkubwa wa bomu katika eneo lenye shughuli nyingi kwenye Mji Mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumamosi, imefikia watu 300 hadi sasa.

Shambulizi la kutisha.
Takriban watu wengine 300 walijeruhiwa kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa (AFP), wakati lori lililokuwa limejazwa vilipuzi lilipolipuka karibu na lango la hoteli.Ahmed Ali, muuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja nchini humo amesema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana. Amesema kuwa miili mingine ilizikwa na jamaa zao.

Wanawake wakipaza sauti.
Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007. Rais Mohamed Abdullahi “Farmajo” Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa shambulizi hilo katili.
“Tumethibitisha kuwa watu 300 waliuawa kwenye mipuko huo. Idasi ya waliokufa huenda bado ikaongezeka na kuna watu kadha ambao bado hawajulikani waliko,” Abdikadir Abdirahman, mkurugenzi wa idara ya magari ya kusafirisha wagonjwa aliliambia shiria la Reuters.