Image result for steve nyerereSteve Nyerere
MCHEKESHAJI maarufu wa Bongo Muvi, Steve Nyerere, amesema kuwa hakuna kitu kibaya kama staa mkubwa kufa akiwa bado yuko kwenye nyumba ya kupanga wakati wana muda sasa wa kujipanga kila mmoja akawa kwenye nyumba yake, kwani gharama wanazotumia mastaa saluni wanaweza kujenga nyumba.
Akizungumza na Kilinge, Steve alisema kuwa wasanii wana uwezo kabisa wa kuwa na nyumba zao lakini wakati mwingine wameweka starehe mbele kuliko maendeleo.
“Jamani ni aibu sana leo staa mkubwa anakufa akiwa kwenye nyumba ya kupanga wakati ana uwezo wa kuwa na nyumba yake mwenyewe, maana hela anazoenda nazo saluni zinatosha kabisa wakizikusanya kwa mwaka na kufanya ujenzi,” alisema Steve.