Mavideo vixer matata kutoka Afrika Mashariki, Vera Sidika wa nchini Kenya na Hamisa Mobetto kutoka Tanzania, wamerushinana maneno kisa video ya Snapchat.

Hamisa ambaye bado yupo nchini Kenya, alitumia mtandao wa Snapchat kujirekodi video akiwa na rafiki kipenzi wa Zari The Boss Lady, baada ya video hiyo kusambaa na kuzua minong’ono ikiwemo maswali ya kwani Vera amegombana na Zari? Hii ni kutokana kuwa binti huyo amekuwa akituhumiwa kutaka kiharibu mahusiano ya kimapenzi kati ya Diamond na Zari.

Kutokana na hali hivyo Vera ameibuka na kuanza kutoa utetezi wake kwa madai kuwa, mrembo wa Tanzania alirekodi video pasipo yeye kujua na wala hakupanga kukutana naye kama inavyo daiwa.

Snapchat za Vera Sidika: