JAJI nchini Uhispania amewazuia rumande viongozi wakuu wawili wa harakati za Uhuru wa Catalonia. Jordi Sánchez, ambaye anaongoza bunge la Catalonia na Jordi Cuixart, kiongozi wa vuguvugu la Omnium Cultural, wanazuiwa huku wakifanyiwa uchunguzi wa uhaini.
Sánchez na Cuixart wanaonekaka kama viongozi wakuu wa kupanga kura ya uhuru wa Jimbo hilo iliyopigwa Oktoba 1, 2017, ambayo hata hivyo ilifutwa na mahakama ya Uhispania. Serikali nchini Uhispania ilitangaza kura hiyo kuwa iko kinyume na sheria.
Kufuatia kura hiyo kiongozi wa eneo la Catalonia Carles Puigdemont, alisaini hatua ya kutangaza uhuru lakini akazuia kutekeleza tangazo hilo. Ametaka mazungumzo kufanyika ndani ya miezi miwili inayokuja.
Hata hivyo serikali ya Uhispania imeonya kuwa Catalonia ni lazima ifute tangazo hilo au ikabiliwe na uongozi wa moja kwa moja kutoka Madrid.
Puigdemont pia ameikasirisha Madrid kwa kukataa kuthibitisha ikiwa ametangaza uhuru au la wiki iliyopita huku akipewa siku hadi Alhamisi kutangaza msimamo wake, aliishambulia serikali katika mtandao wa Twitterkufuatia habari za kuzuiwa kwa Sánchez na Bw. Cuixart’s.