Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo mkoani Geita, Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwafukuza kazi maafisa watatu wa wizara hiyo kutokana na kufanya jaribio la kutaka kuiibia serikali zaidi ya sh. bilioni 29.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dkt Tizeba ambaye yuko mkoani Geita kwaajili ya siku ya maadhimisho ya Chakula duniani. watumishi watatu waliosimamishwa kazi ni Mkurugenzi wa maendeleo ya Mazao, Mkurugenzi wa kitengo cha ununuzi na ugavi, Aliekuwa akikaimu kitengo cha pembejeo
“Hawa sio tu wafukuzwe kazi lakini pia wakamatwe huko popote walipo, watafutwe wakamatwe kwa kuisababishia serikali hasara nimuombe tu IGP nani wawatafute hawajaa watatu hawa, wawatie mbaroni wakatusaidie kusema hizo pesa walifanya mpango gani na hawa watu waliokuwa wanashirikiana nao huko mikoani na wilayani kuuibia umma,” alisema Dkt Tizeba.

“Lakini pia naomba vyombo vya dola vya uchunguzi kuchunguza zaidi na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya watu wote waliohusika katika mpanngo wa ruzuku na katika hili nina maanisha mambo yafuatayo kwasababu ripoti ipo tutawakabidhi wakuu wa mikoa wote nchini ambako mpango wa ruzuku ulikuwa unafanyika.”