Kwa wewe unaefatilia habari za mastaa wa bongo na hasa uhusiano wa Mwimbaji Diamond Platnumz na Zari hivi karibuni utakua umeona meeengi yameandikwa na hata Diamond mwenyewe kukiri kuhusu mtafaruku ulioukumba uhusiano huo.Wengi waliamini kwamba huu ndio unaweza ukawa mwisho wa wawili hawa hasa Zari ambae alionekana kukasirika zaidi baada ya Diamond kukiri kuzaa na Hamisa Mobetto ambapo Zari alifuta picha zote za Diamond pamoja na kutoa kauli zisizopungua 5 zikionyesha dalili za kumalizana na D.

Hata hivyo upepo unaonekana kubadilika baada ya Zari kuanza kuonekana taratibu akiwa na dalili za kurejesha mapenzi yake kwa Diamond Platnumz.
Diamond alipost wimbo mpya wa Harmonize na kutumia mistari hiyo kama dedication kwa Zari ambapo aliandika >>> “We Hodari Mtunza Siri Zangu Hata nikiwa Sina… Hunivumilia na kuamini nitapata… Tafadhali nlindie Roho yangu cha Kukupa sina ila nakuapia Hakiamungu sito kuacha….) Ujumbe wako huo mama@zarithebosslady #SHULALA“
Baada ya hiyo Zari nae alishukuru na kuweka emoji ya kutokwa chozi kutokana na maneno mazito aliyoyaandika Diamond.