Masanamu ya watumwa yaliyopo Kanisani hapo.

Mji Mkongwe wenye historia kubwa unaopatika kisiwa cha Unguja mkoa wa Mjini Magharibi una majengo mengi ya kihistoria kama Beit Ajab, Kanisa la Mkunazini, Ngome kongwe na mengineo ambayo yanayobeba historia nzima kwa mwambao wa Afrika mashariki na kati na tawala za kifalme zilizokuwa zikitumika kuwangonza watu wa visiwa hivyo.

kanisa la Angilakana Mkunazini kwa ndani.

Mji huo ulijipatia umaarufu sana mnamo karne ya kumi 15 mara baada ya kuwa na soko kuu la watumwa kwa Afrika mashariki ambapo watumwa walikuwa wakichukuliwa kutoka maeneo mbali mbali ya Afrika na kupelekwa katika soko kuu la mkunazini na kuuzwa.

Katika vivutio vyote vinavyopatikana Mji mkongwe, Kanisa la mkunazini ni kivutio kikubwa kutokana na historia yake ya kutoka kwenye soko kuu la watumwa kwa mwambao wa afrika mashariki na kati ambapo watu walikuwa wakichukuliwa kutoka maeneo mbali mbali na kufikishwa sokoni hapo na kuuzwa.

Mnamo tarehe 6 ya mwezi wa 6 ya mwaka 1873 hapo ndipo soko kuu la watumwa lilifungwa visiwani Zanzibar na muingeleza ingawa biashara hiyo iliendelea kwa siri katika maeneo mengine mpaka mwaka 1907 hapo ndipo biashara ilisimamishwa rasmi.

Mara baaada ya kusitishwa rasmi kwa biashara ya utumwa Padrii Edward stear aliweza kulitumia eneo hilo la mkunazini ambapo awali kulikuwa eneo la soko la watumwa kwa alianzisha ujenzi wa kanisa la dhehebu la Angalikana mnamo mwaka 1873 mpaka 1880 kwa lengo la kuwakomboa waafrika na kueneza mafundisho ya dini ya kikristo.

Baada kukamilika ujenzi wa sehemu takatifu ya kanisa mwaka 1877 ibada ya mwanzo ya kanisa hilo ilifanyika katika kipindi cha sikuu ya Chrismas, ambapo mpaka leo hii kanisa la Mkunazini limekuwa linaendelea na ibada zake na kuwa katika hali ya uimara kutokana na ustadi wa ujenzi uliofanywa toka enzi hizo.