Pale ambapo mapenzi yanafika mwisho na uhusiano kuvunjika huwa inaumiza ambapo inapelekea wengine kuwekeana kinyongo, kutosalimiana au kutotaka kabisa hata kumsikia mwenzake.

Wolper aliwahi kusema kwamba huwa hapendi kumkumbuka na kumpa nafasi Mwanaume alieachana nae haswa Mwanaume aliempenda kisawasawa ila inaonekana sasa hivi maumivu yameondoka na hana kinyongo na Harmonize.

Hata hivyo alitumia Instagram yake kuusifia huo wimbo kwa kuandika “Haka ka nyimbo kazurii sana na video pia ndio usiseme, bwana Raaaaaj umejua kunyoosha, kama bado hujaangalia video ya haka ka wimbo pita kwenye bio ya @Harmonize_tz #uliemchokozakaja #shulala #NaukinibipuTuNakupigia”