Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah Bulembo amewapongeza viongozi wote wa chama hicho kwa kushiriki kikamilifu hadi kufikia kuanza ujenzi wa ghorofa 14 eneo la Mchikichini.

Hayo Amezungumza leo alipokuwa kwenye Kikao cha jumuiya ya Wazazi ambapo umekutanisha viongozi mbalimbali kutoka mikoa taifa hapa nchini .

Hata hivyo kwenye kikao hicho wamezungumza kuhusu mapendekezo ya viongozi wapya kutokana na wao wanamaliza uongozi wao hivi karibuni.

 

“Nawashukuru sana viongozi mliopo hapa tumekuwa tukishirikiana kwa pamoja katika vitu vingi hata katika jengo letu lilipo Mchikichini nina imani litakuwa jengo zuri na litasaidia sana” amesema.

Amesema leo wamezindua Rasmi ujenzi wa jengo hilo ambalo litakua naofisi za jumuiya ya wazazi na mambo mengine mengi hivyo wanachama hao waendelee kushirikiana na kuwa na umoja kuhakikisha kazi inaenda vizuri na amewatakia kila la heri kwenye uchaguzi.