Zamaradi akiwa na mume wake.
BAADA ya kufunga ndoa hivi karibuni na kuibua gumzo kubwa nchini, aliyekuwa mtangazaji wa Clouds TV, nyepesi vimevuja kuwa baadhi ya wanaotajwa kuwa ndugu zake wanadaiwa wamemsusa.
Akizungumza na Za Motomoto News, mmoja wa ndugu wa karibu wa Zamaradi, aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema ndugu wa upande wa baba yake hawako naye vizuri kwani wanadai hawakushirikishwa wala kualikwa katika shughuli hiyo, kitendo ambacho kiliwakasirisha.
Lakini Zamaradi alipoulizwa kuhusiana na hilo alisema; “Hakuna kitu kama hicho, kwani waliokuwa ndugu zangu wote niliwaalika na walihudhuria kwenye ndoa yangu.”