Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga
leo tarehe 18 Oktoba, 2017 ameripoti rasmi Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo
Mtaa wa Kilimani, Makao Makuu ya Nchi, Mjini Dodoma.
 
Mhe. Hasunga amepokelewa na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na kuingia ofisini
kwake kwa mara ya kwanza ambapo amesaini kitabu cha wageni na baadaye akapata
fursa ya kuzungumza na watumishi wa Wizara hiyo waliopo Dodoma.
 
Akizungumza na watumishi
hao baada ya kutambulishwa, Mhe. Hasunga aliwaomba ushirikiano katika
kufanikisha majukumu ya Wizara ambayo ni kuhifadhi na kusimamia matumizi
endelevu ya maliasili na malikale, na kuendeleza ufugaji nyuki na utalii.
 
“Nawaombeni ushirikiano
tufanye kazi kama timu na tutekeleze majukumu yale ambayo tumepewa, nadhani kwa
ushirikiano kwa pamoja tutaweza”. Alisema Mhe. Hasunga.
 
Naibu Waziri Hasunga ni
mingoni mwa mawaziri wapya walioteuliwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na
kuapishwa Oktoba 9, 2017 baada ya kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
Awali nafasi hiyo ilikuwa imeshikiliwa na Mhe. Mhandisi Ramo Makani.
 
Aidha, katika uteuzi huo,
Dkt. Magufuli alimteua pia Mhe. Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla kuwa Waziri wa
Wizara hiyo akichukua nafasi ya Mhe. Prof. Jumanne Maghembe. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto)
akikaribishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati)
alipowasili kwa mara ya kwanza katika ofisi ya makao makuu ya wizara hiyo zilizopo
mtaa wa Kilimani mjini Dodoma leo. Kulia anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala na Rasilimali Watu, Tutubi Mangazeni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence
Milanzi (kushoto) akimtambulisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet
Hasunga (kulia) kwa watumishi wa Wizara hiyo kabla ya kuzungumza nao leo mjini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto)
akizungumza na baadhi ya watumishi wa wizara hiyo baada ya kuwasili kwa mara ya
kwanza katika ofisi ya makao makuu ya wizara hiyo zilizopo mtaa wa Kilimani mjini
Dodoma leo. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na baadhi ya watumishi wa wizara hiyo baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza katika ofisi ya makao makuu ya wizara hiyo zilizopo mtaa wa Kilimani mjini Dodoma leo. 
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet Hasunga (hayuko pichani).
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Japhet Hasunga (hayuko pichani).