Ofisi ya kupambana na uhamiaji haramu ya mji wa Sabratha ulioko magharibi mwa Libya imesema, hivi karibuni serikali ya mji huo imewarejesha wakimbizi haramu 7,000 hivi.
Ofisi hiyo imetoa taarifa ikisema, imeshirikiana na kikosi cha usalama cha mji wa Sabratha kukagua vituo vya kuwapokea wakimbizi haramu. Taarifa hiyo imefafanua kuwa, wakimbizi haramu 7,428 waliorejeshwa ni pamoja na wajawazito na watoto, ambao wengi wao wanatoka nchi za kiarabu, nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Sahara na baadhi ya nchi za Asia.
Tangu mwaka 2011, hali ya usalama ya Libya inazidi kuwa mbaya, serikali imeshindwa kusimamia kwa ufanisi maeneo ya mipaka ya bahari, na baadhi ya wakimbizi haramu wanaitumia Libya kama kituo cha kuhamia nchi za Ulaya.