Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema Tanzania na Nchi ya Oman wamefanya mazungumzo ya pamoja ya namna ya kukuza sekta ya Utalii baina ya nchi hizo mbili ambapo watashirikiana katika muingiliano wa Watalii watakaokuwa wakitokea moja kwa moja Oman na kuja Tanzania.Tumeweza kuzungumzia ushirikiano wa sekta ya Utalii. Hii ni pamoja na kuanzisha soko la pamoja kati ya Oman na Tanzania. Watalii wanaokwenda Oman wanaotaka kuja nchi za Afrika basi waunganishwe moja kwa moja kutoka Oman na kuja Tanzania kwani wenzetu wana watalii wengi kuliko sisi. Hivyo ujio wao hapa nchini ni faida kubwa kabisa na tumejifunza mengi katika sekta hii.Pia tumeweza kujifunza namna wenzetu wanavyoitangaza nchi yao na sisi tutatumia uzoefu huo kuboresha sekta hii ya Utalii kama dhamana tuliyopewa” alieleza Dk. Kigwangalla.
Awali Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika mapema jana Jijini Dar e Salaam ikiwa katika msafara wa kitaifa kati ya Serikali ya Oman na Tanzania.
Aidha, katika tukio hilo Mh. Waziri DK. Kigwangalla aliweza kuungana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu Hassan katika chakula cha mchana ndani ya Meli hiyo ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’.
Meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ ipo nchini hadi Oktoba 21.2017. ambapo ipo nchini kusambaza ujumbe wa ‘Amani na upendo’ duniani ambapo ikitoka Tanzania inatarajia kuelekea Mombasa Kenya kwa madhumuni hayo hayo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi wakati Dk. Kigwangalla alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman iliyopo nchini.

Moja ya alama za kuvutia za Taifa la Oman

Moja ya usafiri unatumika katika nyanja za Utalii nchini Oman

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi wakati Dk. Kigwangalla alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman iliyopo nchini.

Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi akitoa maelezo kwa Waziri wa Maliasili Dk. Kigwangalla alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman iliyopo nchini.

Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kumaliza kwa tukio la chakula cha mchana ndani ya meli ya Mfalme wa Oman, mapema leo Jijini Dar e Salaam.

Waziri Maliasili na Utalii DK. Kigwangalla akizungumza katika tukio hilomara baada ya chakula cha mchana ndani ya Meli ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’.

Waziri Maliasili na Utalii DK. Kigwangalla akizungumza katika tukio hilomara baada ya chakula cha mchana ndani ya Meli ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’. Chini meli hiyo.