Moja ya mikakati ambayo Chama cha Kikomunisti China (CPC) imeipa kipaumbele ni vita dhidi ya rushwa, na katika mkutano wake mkuu unaoendelea jijini hapa, kimetangaza kufuatilia uozo huo katika milango ya watu.Naibu Katibu wa Tume Kuu ya CPC ya Nidhamu na Ukaguzi, Yang Xiaodu akizungumza na waandishi wa habari amesema chama hicho kitaendelea kupambana na rushwa kwa nguvu zote na hakitamvumilia yeyote atakayebainika kushiriki katika rushwa.
Amesema leo Alhamisi Oktoba 19,2017 kuwa licha ya kufuatilia vitendo vya rushwa katika kona mbalimbali ikiwemo majumbani, wataendelea kuwafuatilia waliokimbilia ng’ambo na kutwaa mali walizochuma isivyo halali.